Alhamisi 1 Januari 2026 - 01:28
Tadhari kutoka kwa mtafiti wa siasa kuhusiana na hali ya kutisha inayotawala Syria; wachache wanazidi kumalizwa taratibu

Hawza/ Iyas Al-Khatib alisisitiza kuwa kile kinachoonekana leo, maandamano na madai ya haki ya kujitawala na kulinda heshima katika miji ya Tartus na Latakia ni matokeo ya kiasili.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Iyas Al-Khatib, mtafiti na mhadhiri wa chuo kikuu, alisisitiza kuwa kile kinachoonekana leo, maandamano na madai ya haki ya kujiamulia hatima na kulinda heshima huko Tartus na Latakia ni matokeo ya kiasili, na kinaonesha kuwa serikali hii tangu mwanzo wa kuingia kwake Syria, imejitahidi kuondoa heshima ya kitaifa ya Wasyria.

Al-Khatib, akirejea kuwa matukio ya sasa katika pwani ya Syria ni mwendelezo wa mabadiliko ya awali huko As-Suwayda na kaskazini mashariki mwa mto Furati, alisisitiza kuwa Wa-Alawi wako katika mazingira ya ukandamizwaji mkubwa, huku habari hiyo ikifunikwa kwa kiwango kikubwa na utawala wa Al-Jolani juu ya kila kinachowakumba.

Alieleza kuwa vielelezo vingi vya uhalisia wa matukio bado vimebaki katika ngazi ya ndani na, kutokana na shinikizo la serikali, vimeshindwa kusambazwa kwa umma; mtu yeyote anayetaka kurekodi picha au video hukumbana na vikwazo na vitisho.

Al-Khatib aliongeza kusema: Kila siku huzuiwa taarifa, na hata majina ya vijana na hata watoto wa kiume, ambao wanauawa kwa makusudi katika eneo la pwani, bila serikali kutoa tamko lolote kuhusu hilo. Mtafiti huyu wa siasa alibainisha kuwa matukio ya mauaji ya kila siku yanaendelea huko Tartus, Latakia, Baniyas, Jableh, vijiji vya Homs Magharibi na vijiji vya Hama Magharibi, na wakati mwingine idadi ya waathiriwa hawa hufikia makumi ya watu.

Ikumbukwe kuwa maandamano haya yalifanyika kwa kuitikia wito wa Sheikh Ghazal Ghazal, Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Wa-Alawi ndani na nje ya Syria, wa kuandaa maandamano ya amani.

Washiriki wa maandamano walipaza sauti kaulimbiu zenye ujumbe usemao “simamisheni mauaji na umwagaji damu”, wakadai haki na uadilifu, wakilaani kulipuliwa Msikiti wa Imam Ali bin Abi Talib (amani iwe juu yake) huko Homs Ijumaa iliyopita, na pia wakataka kuachiliwa watu wote waliokamatwa baada ya kuanguka kwa serikali ya awali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha